ANA WATOTO WENGI MPAKA HAWAJUI MAJINA YAO.



Musa Hasahya, mwanaume mwenye umri wa miaka 68 kutoka Uganda, amekuwa gumzo baada ya kufichua kuwa ana wake 12 na watoto 102. Hasahya anakiri kuwa mara nyingi husahau majina ya watoto wake kutokana na idadi yao kuwa kubwa kupindukia.

Akihojiwa, Hasahya alisema: “Mapato yangu yamepungua sana kadri maisha yanavyozidi kuwa magumu, lakini familia yangu imekuwa kubwa na kubwa. Niliendelea kuoa mke baada ya mwingine. Mwanaume anawezaje kuridhika na mke mmoja?”

Hata hivyo, sasa mambo yamebadilika. Wake zake wote wamewekwa kwenye mpango wa uzazi wa mpango, na Hasahya anasema amefikia kikomo cha kuongeza familia. Hili linakuja wakati gharama za maisha nchini humo zikizidi kupanda, na mzigo wa kulea familia kubwa ukizidi kuwa mgumu kubeba.

Kisa chake kimezua mijadala kuhusu uzazi wa mpango, majukumu ya kifamilia, na changamoto za maisha ya kisasa.

Je, unapanga mwisho wako kuwa watoto wangapi?

Comments

Popular posts from this blog

From Lecture Halls to Hustle: The Inspiring Story of Haggai, the Student Entrepreneur of Kibabii University

Hidden secrets behind namaloko area. One of the most fearful places around kibabii university.